SERA YA HISA
MAANA YA HISA
Hisa ni kiasi cha fedha ambacho mwanachama anapaswa kuweka katika chama kwa mujibu wa masharti kwa lengo la kuhimarisha mtaji wa chama.
MADHUMUNI YA HISA
Madhumuni au malengo ya hisa ni kuhakikisha kuwa kila mwanachama anakuwa na haki sawa katika kumiliki chama kwa mujibu wa masharti ya chama na bila kuvunja sheria kuu ya ushirika.
NAMNA YA UCHANGIAJI WA HISA
Masharti ya chama sehemu ya 4, kifungu namba 14 (1(b)) kinaeleza namna ya kuweka hisa na kwa kuzingatia marekebisho yaliyofanywa na mkutano maalum wa mwaka 2023. Aidha kila mwanachama anapaswa kuwa na hisa ishirini na tano zenye thamani ya TZS 20,000/= (Elfu ishirini) kila hisa moja. Jumla TZS 500,000/= (Laki tano). Mwanachama mpya atachangia si chini ya TZS 50,000/= (Elfu hamsinii) kila mwezi kwa muda wa miezi kumi ili hatimize hisa ishirini na tano zenye jumla ya TZS 500,000/= (Laki tano).
HISA KAMA HAKI
Kulingana na madhumuni ya hisa kama yalivyoainishwa, hisa itabaki kama haki na dhamana ya mwanachama katika chama na haitatolewa faida.