SERA YA AMANA

 MAANA YA AMANA

Amana ni akiba au mawekezo yanayowekwa na mwanachama kwa nia ya kutunza kwa muda maalum wa miezi mitatu, miezi sita, miezi tisa au mwaka mmoja.  zinaweza kuchukuliwa pindi muda ulioainishwa kutimia kwa kuzingatia aina ya amana.

 

 MADHUMUNI YA SERA YA AMANA

Madhumuni ya sera hii ni kuwawezesha wanachama kutatua changamoto mbalimbali za kijamii kwa njia rahisi na kuepuka ulazima wa kutumia mikopo kutatulia changamoto hizo za kijamii kama kulipia ada za shule, gharama za matibabu, likizo maandalizi ya sikukuu au sherehe n.k

 

AINA ZA AMANA

 

 (i) Amana ya hiyari (Elimu, likizo, sikukuu/sherehe)

a)    Mwanachama ataweka kiasi cha fedha mara kwa mara kwa kadri ya uwezo wake na kuzichukua muda wa kulipa ada za shule unapowadia, muda wa likizo, sikukuu na sherehe kwa mujibu wa makubaliano kati yake na chama ambayo ni lazima yawe katika vipindi maalum vya miezi mitatu (3), miezi sita (6), miezi tisa (9) au miezi kumi na mbili (12)

 

b)    Katika uwekezaji wa amana kima cha chini ni TZS 50,000 (Elfu hamsini) ambapo mwanachama husika hatalazimika kupeleka fedha hizo benki na kuwasilisha slip kwenye ofisi ya chama au kukatwa moja kwa moja kwenye stahiki zake za kila mwezi bila kuathiri uchangia wa akiba za kila mwezi pamoja na marejesho ya mkopo kama mwanachama husika ana mkopo chamani.

 

c)    Amana hii itawekewa faida ya asilimia sita (6%) kwa mwaka kwa kufuata kanuni hii:

 

                               Faida = A x R X N

 

Ambapo:

A =Kiasi cha Amana

n= Muda wa miezi katika mwaka (mfano, miezi 3, miezi 6 au muda wa mwaka n=12)

R= Riba kwa mwezi ambayo ni TZS 0.5

 

 

 (ii) Amana ya kustaafu

a) Mwanachama ataweka kiasi cha fedha mara kwa mara kwa kadri ya uwezo wake na kuzichukua kwa mujibu wa makubaliano kati yake na chama ambayo ni lazima yawe katika kipindi maalum cha miaka miwili, ambapo riba yake itakokotolewa kila baada ya mwaka mmoja.

 

b) Katika uwekezaji wa amana kima cha chini ni TZS 50,000 (Elfu hamsini) ambapo mwanachama husika hatalazimika kupeleka fedha hizo benki na kuwasilisha slip kwenye ofisi ya chama au kukatwa moja kwa moja kwenye posho yake ya kila mwezi bila kuathiri uchangia wa akiba za kila mwezi pamoja na marejesho ya mkopo kama mwanachama husika ana mkopo chamani.

 

a)    Amana hii itawekewa faida ya asilimia nane (8%) kwa mwaka kwa kufuata kanuni hii:

 

                               Faida = A x R X N

Ambapo:

A =Kiasi cha Amana

n= Muda wa miezi katika mwaka (n=12)

R= Riba kwa mwaka 8%

 

         UTARATIBU WA KUCHUKUA AMANA

 

Kabla amana hazijachukuliwa utaratibu ufuatao ni lazima ufuatwe:

 

 (i) Mwanachama husika atajaza fomu maalum itakayoonyesha kiasi cha amana    

     kinachochukuliwa kwa namba na maneno.

 

(ii) Mwanachama husika ataeleza aina ya amana anayoichukuwa baada ya kukidhi vigezo         vya muda wa amana husika

 

(iii) Mwanachama atakayechukua amana zake kabla ya muda wa makubaliano kufika

      hatopata faida ya vipindi vilivyo nje ya makubalano 

 UTHIBITISHO

Sera hii imethibitishwa, kusomwa, kujadiliwa na kukubaliwa na Mkutano Mkuu maalum wa

 

 Wanachama wote wa Viwango SACCOS uliofanyika tarehe 14-10-2023 na mkutano mkuu wa mwaka 2023 uliofanyika tarehe 09-12-2023

 

KAULI MBIU: KOPA KWA BUSARA LIPA KWA WAKATI.