TAARIFA YA HABARI YA MKUTANO MKUU 2025
SIMU: 0713557846 / 0719041634 / 0676203880
TAARIFA YA HABARI YA MKUTANO MKUU 2025
MKUTANO WA MAFUNZO KWA WANACHAMA WA VIWANGO SACCOS LTD KWA MWAKA 2025
Ndugu wanachama,
Uongozi wa chama Viwango SACCOS LTD unapenda kuwajulisha kwa furaha na fahari kubwa kwamba chama kimefanikiwa kupata tuzo ya heshima kutokana na jitihada na mchango wake katika sekta ya Ushirika.
Tuzo hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo chakula na Ushirika ikishuhudiwa na mwakilishi wa Benki kuu ya Tanzania ( BOT) pamoja na Mrajis wa vyama vya Ushirika Tanzania, katika hafla ya Uzinduzi wa taarifa ya utendaji wa vyama vya Ushirika (SACCOS) mwaka 2024, iliyofanyika LUSH GARDEN HOTEL, ARUSHA tarehe 29 Septemba 2025.
Aidha, chama chetu kimefanikiwa pia kuingia kwenye vipengele mbalimbali vya ubora kwa SACCOS bora 20 kwenye utoaji wa mikopo pamoja na ukusanyaji mapato, hatua inayoonesha uthibitisho wa kazi nzuri, mshikamano wa wanachama na dhamira ya kuendelea kutoa huduma bora zaidi.
Tuzo hii ni ushindi wa kila mwanachama, na ni matunda ya mshikamano, ushirikiano na kujitolea kwa dhati. Tunaamini huu ni mwanzo wa mafanikio makubwa zaidi yanayokuja mbele yetu.
Tunaendelea kuwasihi wanachama wote kuendeleza mshikamano, nidhamu na juhudi ili tuzidi kuimarisha hadhi ya chama chetu.
Hongera kwetu sote!
Imetolewa na
CPA-Khalid Kibwana
MENEJA-VIWANGO SACCOS LTD
MKUTANO MKUU WA 38
2024
02 NOV 2024
TBS UBUNGO (HQ)
28 SEPT 2024
TBS UBUNGO (HQ)
28 SEPT 2024
TBS UBUNGO (HQ)
28 SEPT 2024
28 - 09 - 2024