SERA YA AKIBA

 

   MAANA YA AKIBA

Akiba ni kiasi cha fedha ambacho mwanachama anaweka katika chama ikiwa kama ni mawekezo na anatumia kama dhamana wakati wa kukopa.

 

 MADHUMUNI YA AKIBA

Akiba hutumika kama dhamana kwa wanachama wakati wa kukopa kwa mujibu wa taratibu na kanuni za mkopo husika.

 

 UWEKAJI WA AKIBA

Kwa mujibu wa masharti ya chama kifungu namba 14 (c) na kifungu 28 (1), mwanachama ana wajibu wa kuweka kiasi cha fedha kisichopungua TZS 200,000/= (Laki mbili) kila mwezi kama akiba yake.Aidha kiasi hicho kwa mujibu wa kifungu namba 14 (c) cha masharti ya chama kinaweza kubadilika. Hata hivyo mwanachama anaweza kuweka kiasi chochote zaidi ya TZS 200,000/= wakati wowote anapotaka kama akiba yake katika chama

 

 FAIDA JUU YA AKIBA

Chama kitakuwa kinatoa faida juu ya akiba za wanachama kila mwaka wa fedha kutoka kwenye ziada yake kwa asilimia kati ya 0 hadi 50%. Mkutano mkuu utafanya maamuzi ya mwisho kuhusu kiwango cha faida juu ya akiba kitakachogawiwa kwa wanachama kama ilivyoelezwa kwenye kanuni za asasi ndogo za fedha za mwaka 2019 kifungu namba 22 (1) na kwenye masharti ya chama kifungu cha 28 (6), ambapo ukokotozi wake utafanyika kila robo mwaka na kuhusisha wanachama hai.

 

  UTARATIBU WA KUHAMISHA AKIBA

Katika kipindi hiki cha mpito ambacho chama kinachangamoto ya ukwasi, Mwanachama HATORUHUSIWA kupunguza akiba zake mpaka hapo utaratibu mpya utakapoainishwa, ambapo utaratibu utazingatia uwiano wa akiba na mikopo ya mwanachama husika.